Latest News

MH RAIS J.M.KIKWETE ATEUA MABALOZI WAPYA SITA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Mabalozi sita kushika nyadhifa mbalimbali nje ya nchi .

Katika uteuzi huo, Rais amemteua Balozi Mohamed Mwinyi Haji Mzale kuwa Balozi wa Tanzania huko Stockhlm Sweden kushika nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ben Moses aliyestaafu utumishi wa umma. Kabla ya uteuzi huo, Balozi Mzale alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha habari zaidi zinasema kuwa Rais amemteua Balozi Elexander Massinda kuwa Balozi wa Tanzania huko Ottawa nchini Canada kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Allan Kallaghe aliyetuliwa kuwa Balozi wa Tanzania huko London .

Kabla ya uteuzi huo Balozi Massinda alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Balozi Kallaghe anachukua nafasi ya Balozi Mwanaidi Sinare Maajar ambaye mapema mwaka huu Rais alimteua kuwa Balozi wa Tanzania huko Washington DC, Marekani.

Habari zinasema kuwa balozi wa Tanzania huko Brasilia,Balozi Dkt. Joram Mkama Biswaro ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Addis Ababa na Umoja wa Afrika. Balozi Dkt. Mohamed Omar Maundi anakuwa Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia (CFR) Dar es Salaam.

Rais pia amemteua Balozi Begun Karim-Taj kuwa Balozi wa Tanzania huko Paris, Ufaransa, ambapo anachukua nafasi iliyoachwa na Balozi Hassan Gumbo Kibelloh aliyestaafu. Kabla ya uteuzi huo Balozi Taj alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply