Latest News

‘JAM SESSION’ YAZINDULIWA SUN CIRRO

Michael Ross akifanya makamuzi ya nguvu katika uzinduzi huo.
ULE mpango mzima unaohusisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam ambao unajulikana kama ‘Jam Session’ ambapo wanafunzi watakuwa wakikutanika na kucheza miziki na sarakasi, jana ulizinduliwa rasmi ndani ya ukumbi wa klabu ya Sun Cirro uliopo maeneo ya Legho, Sinza, jijini Dar es Salaam, kwa onyesho lililofanywa na msanii kutoka nchini Uganda, Michael Ross.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali nchini wanamuziki Witness, AY na wasanii wa filamu, Dokii na Jacky wa Chuzi ambapo Jack Pemba alikiwa miongoni mwa wageni wa heshima. Hafla hiyo ilishereheshwa na mtangazaji mahiri kutoka redio ya Clouds FM, Hamisi Mandi ‘B12’.
Witness naye hakuwa nyuma kuonyesha vitu vyake muda mfupi baada ya kupanda jukwaani.
Mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds FM ‘B12’ akiongea jambo katika shughuli hizo.
Witness akiwa na mmoja wa wadau wa Jam Session.
Ambwene Yesaya ‘AY’ (wa pili kushoto) akiwa na mashabiki wake Club Sun Cirro.
Michael Ross (kulia) katika pozi na mmoja wa washiriki wa Jam Session.
DJ Choka (kushoto) akipiga stori na Michael Ross muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani.
Jack Pemba (kushoto) akiwa na meneja wa Michael Ross aitwaye Aly Allibhai.
Witness katika pozi na MC wa Jam Session.
Dokii akiwa katika pozi la hatari wakati wa mchakato mzima wa upigaji wa picha ndani ya Sun Cirro.
Jaqueline Pentezel akiunda pozi na mdau wa Jam Session.

Picha: Musa Mateja /GPL
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply