Latest News

KAMBI YA REDDS MISS ILALA -2010

Mwandaaji wa Miss Ilala Jackson Kalikumtima akifafanua jambo. Shoto ni Miss Ilala 2009 Sylvia Shally. Chini warembo wakiwa na waandaaji
Shindano la kumtatafuta Mrembo wa Kanda ya Ilala mwaka huu litajulikana kuwa ni REDDS MISS ILALA 2010 na litashirikisha warembo 18 ambao wametoka kwenye vitongoji mbali mbali vilivyoko katika Manispaa ya Ilala. Warembo walianza Mazoezi wiki moja iliyopita hapa katika Hotel Apartment ya Lamada chini ya Waalimu Wanne Star anayefundisha kucheza na ku kulitawala jukwaa. Leila Bhanji anawafundisha kutembea, kujiamini na kujitunza.

Pia tumekuwa tukikaribisha Wataalamu wa mambo mbali mbali kuja kuwasaidia washiriki wetu ili wawe tayari kimwili na kisaikolojia kwa ajili ya shindano la Redds Miss Ilala 2010 litakalo fanyika Ubungo Plaza tarehe 26 Juni.

Pia Ruge Mutahaba alikuwepo kusaidia kutoa somo kuhusu vipaji na namna ya kujitambua na kukuza vipaji. Leo tutakuwa na Maafisa wa Manispaa ya Ilala ambao wataendesha mafunzo mbali mbali ya Uzalendo kwa warembo ili waijue Manispaa yao, mkoa wao na nchi yao nzuri ya Tanzania. Mashindano ya mwaka huu ya kumtafuta Mrembo atakaye beba Bendera ya Manispaa ya Ilala yatakuwa tofauti na mashindano tuliyozoea. Kuna vipengere ambavyo sisi waandaji tumevibuni na kuviongeza ili kunogesha shindano hilo na kulifanya libaki katika kumbukumbu ya mashindano bora yaliyowahi kufanyika hapa Tanzania. Warembo walooko kwenye kambi ya Redds Miss Ilala 2010 ni 18 kusimamiwa na Sylivia Shally ambaye ni Miss Ilala anaye maliza muda wake.

Warembo hao ni salma Mwakalukwa, Doreen Mutabingwa, sarah Nalolah, Joyce Sadick, lilian Massam, Cinthia Bavo, Consolatha Lukosi, Ritha Swai, Happiness Mushi, Ummy Mohamed, Neema Jacob, Harrieth Mulumba, Sanza Mukajanga, Agness Francis, Mariam Kimario, Neema Allen, Bahati Chando, Celine Wangusu. Mwaka jana kanda ya Ilala pamoja na kutokufanikiwa kushinda Taji la Miss Tanzania ilifanya vizuri sana na kuvunja rekodi mbili kwenye historia ya mashindano ya Miss Tanzania. Kwa kufanya hivyo, kampuni ya Dar Metropolitan Promotions ambayo ndiyo imekuwa ikiandaa mashindano ya Miss Ilala kwa miaka 12 sasaikawa imejiongezea rekodi zake kwenye mashindano haya. Rekodi zilizovunjwa mwaka jana · Kwa mara ya kwanza Kanda moja iliingiza Warembo watano kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Mrembo wa Tanzania. Kwa kawaida na kwa kufuata kanuni ni warembo watatu tu wanaoingia kwenye Kambi ya Miss Tanzania kutoka kila Kanda.

Kwa UBORA WA WAREMBO WA ILALA mwaka jana:

.Warembo watano walichaguliwa kuiwakilisha kanda ya ilala.
· Warembo wanne wa miss ilala waliingia kwenye kumi bora ya miss tanzania na kulifanya shindano kuwa

Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply