Latest News

News alert: Maisha club kufunguliwa wiki hii

New Maisha Club kuzinduliwa kesho
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EML Francis Anthony Ciza Majey akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa Club maisha mapema leo asubuhi,shoto ni meneja wa club hiyo Allan Ngugi
Moja ya sehemu mbili za Ma DJ
Kila sehemu kumetakata
Mlango wa kuingilia New Maisha Club iliyoko Oysterbay jijini Dar umewekwa 'ChwiChwiChwi' (metal detector) kujihami na uingiaji na silaha ama chuma
New Maisha Club kwa nje. Bwawa la kuogelea halipo tena hapo mbele
sehemu ya juu ndani ya New Maisha Club
Sehemu ya ndani
ukumbi wa kusakatia libeneke. New Maisha Club iliyokuwa Maisha Club kabla ya kuteketea kwa moto mnamo Novemba 8 mwaka jana inafungua milango kwa wadau kuanzia kesho ambapo sherehe ya uzinduzi kukata na shoka inaandaliwa. Kwa wale ambao hawakuona habari ya awali ya kuungua kwa Maisha club ama wanaotaka kujikumbushia:
BOFYA HAPA

UKUMBI maarufu wa starehe wa Club Maisha unatarajiwa kufunguliwa upya Juni 24 mwaka huu, baada ya kufanyiwa ujenzi mkubwa kutokana na kuungua moto mwaka jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Majey), alisema klabu hiyo imefanyiwa ubunifu mkubwa ili kukonga nyoyo kwa kutoa burudani murua na ya uhakika kwa wateja wake.

“Club Maisha inakuja katika mtazamo mpya kwa kutoa burudani za usiku Dar es Salaam iliyopambwa vizuri, sauti ya kutosha na inaipeleka Tanzania mbele katika kutoa burudani za usiku.

“Baada ya miezi kadhaa wateja wetu kukosa burudani, klabu yao sasa inarudi ikiwa ni ya kisasa zaidi yenye televisheni 32 zitakazokuwa zikionesha fainali za Kombe la Dunia na video za muziki, sehemu mbili za kuchezea, vyumba viwili maalumu vya VIP, hii yote ni katika kuuweka kuwa ya kisasa,” alisema Majey.

Vitu vingine vilivyopo katika Club Maisha ni pamoja na sehemu za kuvutia sigara, varanda ya juu, sehemu saba (7) za baa, jiko na TV kubwa inayoonesha fainali za Kombe la Dunia na michezo mingine kwa nje.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema siku itakayofunguliwa Club Maisha itakolezwa na kusisimuliwa na baadhi ya wachezeshaji muziki (ma-DJ) kutoka Afrika Mashariki na Marekani ambao watapiga nyimbo kali zinazotesa kwa sasa duniani.

“Klabu tayari imekaguliwa na mainjinia kutoka Idara ya Zimamoto pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kuhakikisha hakuna ajali ya moto inayoweza kutokea tena, na milango ya dharura imeongezwa ili kuhakikisha usalama mkubwa unakuwepo,” alisema Majey.

“Tumewekeza vya kutosha ili kuirejesha Club Maisha katika nafasi yake ya ubora kwa klabu za usiku Tanzani, tumeweka staili za kisasa kwa lengo la kutoa burudani iliyotakata kwa wapenda burudani za usiku,” alisema.

Viingilio vitabaki kuwa vya kawaida ambavyo
ni sh. 10,000 sehemu ya kawaida na sh. 20,000 kwa VIP.
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply