Latest News

More latest news

Editor's picks

WORLD

US

Entertainment

Business

  • The £140m flat: World-record price earns mystery buyer room service f...Read more

Sports

  • Mario Balotelli's double life: The bitter family feud that haunts the...Read more

Technology

. Newcastle yatupa ndoano kwa Ulimwengu

Thomas Ulimwengu alipokuwa akihojiwa na wanahabari kabla ya kwenda Sweden.

KLABU kongwe inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Newcastle FC imeonyesha nia ya wazi kutaka kumchukua mshambuliaji kinda Mtanzania, Thomas Ulimwengu.

Newcastle FC ambayo ni moja ya timu kubwa na yenye heshima kubwa nchini England, tayari imefanya mazungumzo ya awali na Shule ya Soka ya AFC ya nchini Sweden ili ikiwezekana kinda huyo atue England kwenye timu ya watoto ya timu hiyo.

Mmiliki wa shule ya kukuza na kuendeleza vipaji ya AFC, Alex Ryssholm ameliambia Championi Jumatatu kutoka Stockholm, Sweden kwamba wataalamu wa kukagua vipaji wa Newcastle walivutiwa na uwezo wa Ulimwengu wakati wa michuano ya Gothia Cup.

“Tuliishia robo fainali, Thomas alicheza mechi zote nne, alifunga mabao saba. Wameonyeshwa kuvutiwa naye, lakini hata hivyo inabidi wavute subira kwa kuwa bado si mchezaji wetu rasmi.

“Tunatakiwa kukamilisha taratibu na TSA, iko chini ya Shirikisho la Soka la Tanzania. Baada ya hapo tunaweza kuzungumza nao, tayari tumewasiliana na wakala aitwaye, Damas Ndumbaro na analifanyia kazi ikiwezekana tulikamilishe mapema,” alisema Ryssholm.

Ryssholm alisema binafsi amevutiwa na kipaji cha Ulimwengu na Watanzania wengine wawili walio katika shule yake hiyo ambayo imekuwa ikifanikiwa kukuza vipaji na kuwapatia nafasi makinda hao kucheza kwenye timu kubwa za Ulaya.

Ulimwengu alitarajia kutua nchini jana kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes ambayo itacheza mechi ya marudiano dhidi ya Ivory Coast kuwania kufuzu katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana.

Mechi ya kwanza, Heroes ikiwa ugenini jijini Abidjan ililala kwa bao 1-0, maana yake inatakiwa kupata ushindi wa mabao mawili au zaidi na kuhakikisha pia nyavu zake haziguswi katika mechi hiyi itakayochezwa Jumamosi ijayo.

Source by Global
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply