Jan Paulsen (kulia) akiwapa maelekezo wachezaji wa Stars. Kulia kwake ni msaidizi wake Silvester Marsh.
Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Jan Paulsen aliyerithi nafasi ya Mbrazili Marcio Maximo, aliyeanza kazi na timu hiyo jana, leo aliendelea kuinoa timu hiyo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars.
….akiandaa uwanja kwa ajili ya zoezi maalum.
Akimuelekeza jambo kipa wa timu hiyo, Juma Kaseja.
Athumani Iddi Chuji (kushoto) na Juma Kaseja, wakifanya mazoezi kwenye kikosi hicho.
Juma Kaseja akionesha cheche zake kwenye mazoezi hayo.
Abdi Kassim (kushoto) na Athumani Iddi Chuji, wakijifua mbele ya Jan Paulsen.
Jan Paulsen akimfundisha beki wa Timu hiyo, Shadrack Nsajigwa jinsi ya kumzuia adui.
Sehemu ya umati wa watu uliofurika kushuhudia mazoezi hayo leo asubuhi.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL
Source by Global
0 comments