Latest News

Fally Ipupa amnasa Keri Hilson
                      
BAADA ya kupata mafaniko kwenye ngoma ya Chaise electrique aliyomshirikisha First Lady wa zamani wa G-Unit, Olivia Longott, staa wa Soukouss kutoka pande za Congo DR, Francois Ipupa Nsimba ‘Fally Ipupa de Caprio’, ameweka kweupe mpango wake wa kugonga ngoma na mkali wa R&B huko mtoni, Keri Hilson.

Fally aliuambia mtandao wa Congo Planet.com kuwa, alikutana na Keri kwa mara ya kwanza mwezi jana huko Afrika Kusini alipokuwa akifanya shoo maalum ya Kombe la Dunia na kuzungumza naye juu ya kugonga ‘kolabo’ ambapo walikubaliana.

“Nilikutana naye Afrika Kusini wakati wa fainali za WOZA, aliniambia anapenda kazi zangu hasa ile niliyofanya na Olivia, sikusita nikamuomba tufanye kazi ya pamoja akakubali hivyo baadaye mwezi huu tutakuwa pamoja Paris, Ufaransa tukikamilisha hilo,” alisema Fally

Source by Mrisho
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply