LADY JAYDEE KUSOMESHA YATIMA WAWILI, WELL DONE KOMANDO
Lady Jaydee (pichani), mwanamuziki na mmiliki wa Machozi Band, Ijumaa hii anatarajia kusherehekea miaka kumi ya kuwa katika muziki katika shoo maluum itakayofanyika pale Millennium Towers-Mzalendo Pub jijini Dar es salaam. Akiongea na media mapema leo katika hoteli ya Paradise City, amesema kuwa ataadhimisha siku hiyo kwa kusomesha pia watoto yatima wawili watakaobahatika kuchaguliwa, ambao watasomeshwa kuanzia kidado cha kwanza hadi cha nne kwa gharama za Machozi Band ikiwa ni njia ya kurejesha shukrani yake kwa jamii na fans wake.
Source by Global
Latest News
0 comments