Latest News

HARTMAN PRODUCTIONS INAWALETEA JAM SESSION



Kampuni ya Hartman Productions yenye ofisi zake maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam , kila Jumapili inafanya project inayoenda kwa jina la Jam Session inayofanyika katika ukumbi wa Club Sun Cirro iliyopo maeneo ya Sinza Legho jijini Darisalaam.
Akizungumza na Blogu hii Mkurugenzi wa Hartman Productions amesema kwamba project hiyo huanza saa nane mchana hadi saa mbili usiku kwakiingilio cha shilingi elfu tatu , shoo yenyewe inalengakutoa jukwaa kwavijana ambao wenye vipaji ili waweze kuonyesha uwezo wao katika kucheza ama kuimba na hadi wakati huu kuna makundi zaidi ya kumi na moja kutoka mashuleni na mitaani.
Aidha, project hii inatoa fursa kwa vijana hawa wanaoinukia kupata fursa ya kukutana na mastaa mbalimbali ambao tayari wamepiga hatua kwenye fani mbalimbali ambapo wiki iliyopita ndani ya nyumbaalikuwepo Steven Kanumba ambaye alionyesha mambo yake na ukumbi mzima kulipuka!!!
Wiki hii inatarajiwa kuwepo Ray na bado kuna mazungumzo yanaendelea ili Ay naye afanye mambo.
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply