Latest News

Eric Shigongo Kuunguruma kwenye mkutano wa diaspora marekani mwezi ujao


Bw. Eric Shigongo

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers & General Enterprises Ltd na mjasiriamali, Bw. Eric Shigongo, anatarajiwa kuhutubia nchini Marekani katika Mkutano maalum ulioandaliwa na Watanzania waishio nchini humo (Diaspora Council of Tanzanians in America - DICOTA).


Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia Julai 1, mwaka huu katika jiji la Minneapolis, Marriott Hotel, Minnesota, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Aman Abeid Karume, amealikwa kuwa mgeni rasmi. Viongozi wengine watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja na maofisa waandamizi na wafanyabishara wakubwa kutoka Serikali ya Tanzania na Marekani.


Aidha, Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Bw. Reginald Abraham Mengi, naye ni miongoni mwa wageni waalikwa wa mkutano huo ambao unafanyika kwa mara ya pili nchini humo ukiwakutanisha Watanzania waishio ughaibuni. Mada mbalimbali zitatolewa na Watanzania waishio ndani na nje ya Marekani.

Mwenyekiti Mtendaji wa Globu ya Jamii, Ankal, naye anategemewa kuwepo kwenye mkutano huu ambao ripoti zinasema watu kibao wamejianddikisha kuhudhuria na wengine wanaendelea kumiminika.

Katika mkutano huo, Bw. Shigongo anatarajiwa kutoa mada itakayoelezea jinsi ya kufanikiwa kiuchumi katika mazingira ya Tanzania na anatarajiwa kuwahamasisha Watanzania waishio ughaibuni kuwekeza nyumbani Tanzania.

Katika siku za hivi karibuni, Bw. Shigongo amejipatia umaarufu kwa kutoa elimu, ushauri kwa vijana na wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu nchini kupitia mikutano na hafla mbalimbali anazoandaa au kualikwa kwa lengo la kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa kitanzania.
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply