Latest News

VITA UWANJANI YAZINDULIWA

Mh.Temba (kushoto)akikamua kwa makini na Chege (kulia)katika uzinduzi huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya Club Sun Cirro.

ALBAMU ya vita Uwanjani inayowahusisha wanamuziki wawili kutoka Kundi la TMK Family, Chege na Mh. Temba jana imezinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Sun Cirro Club uliopo maeneo ya Lego Sinza jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo kulikuwa na wanamuziki kutoka nchini Kenya na Uganda, Wahu na Michael Ross ambao pia walifanya makamuzi ya aina yake na kuvuta hisia za mashabiki waliofurika ukumbini hapo.
Mwanamuzi kutoka nchini Kenya, Wahu akishambulia jukwaa kwa bidii katika uzinduzi wa albamu ya Vita Uwanjani, usiku wa kuamkia leo ndani ya Club Sun Cirro.
Michael Ross wa Uganda akijaribu kuonyesha ujuzi wakewa kuteka jukwaa katika uzinduzi huo.
Michael Ross akitoa tano kwa mashabiki walifurika ukumbini hapo wakati akiendelea kutoa burudani.
Mtangazaji wa Radio Clouds FM, Hamisi Mandi ‘B12’ akitoa tano kwa mashabiki ndani ya Club Sun Cirro ambapo alikuwa mshereheshaji wa Shughuli hiyo.

PICHA ZAIDI

Picha: Musa Mateja/GPL
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply