Latest News

MICHAEL ROSS KUSHEREHESHA ‘MKONO MMOJA’ SUN CIRRO CLUB

Mratibu wa shoo ya ‘Mkono Mmoja’, Fredy Kimiti (kushoto) akiwa na Michael Ross (katikati) na kulia ni Mustapha wa G5 akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau hao maeneo ya Sayansi jijini Dar es Salaam.
MWANAMUZIKI kutoka nchini Uganda, Michael Ross, ametua nchini leo kwa ajili ya kufanya shoo ya uzinduzi wa albamu ya ‘Vita Uwanjani’ ya Chege na Mheshimiwa Temba.

Uzinduzi huo unaokwenda kwa jina la ‘Mkono Mmoja’ utafanyika ndani ya Club Sun Cirro na Michael Ross akiwa mgeni rasmi wa hafla hiyo.
Michael Ross akiwa kwenye gari analotumia kuzungukia likiwa limeegeshwa maeneo ya kituo cha mafuta cha Oil Com maeneo ya Sayansi, Kijitonyama, jijini
Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kutoka kufanya mazoezi kwenye (GYM)
iliyopo eneo hilo.
Baada ya shoo hiyo Michael Ross anatarajia kufanya shoo nyingine siku ya Jumapili Juni 6 wiki hii ambayo itaenda sambamba na uzinduzi wa Jam Session hapohapo Club Sun Cirro.

PICHA: MUSA MATEJA /GPL
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply