Latest News

JACK PEMBA ALIKUWA MGENI RASMI JAM SESSION

PEDESHE wa ukweli kunako pande za burudani mwenye makazi yake nchini Uingereza Jack Pemba hivi juzikati aliibuka Club Sun Cirro iliyopo eneo la Lego Sinza jijini Dar es Salaam katika mchakato mzima wa Jam Session akiwa ndiye mgeni rasmi siku hiyo.

Akiwa katika shughuli hiyo Jack Pemba alipata fursa ya kusaini baadhi ya Tiketi za washiriki wa ishu hiyo na baadaye kupiga nao stori mbili tatu za kuwapa moyo washiriki huku akiwaomba waongeze bidii katika masomo yao ili baadaye waweze kuwa na maisha bora na mazuri kama yake.Baada ya kumaliza kuwapa mawaiza hayo aliwakabidhi waandaaji wa Jam Session iliyo chini ya Hartman Mbilinyi kitita cha Tsh, Milioni moja ikiwa ni moja ya mchango wake baada ya kuvutiwa na maandalizi ya mpango huo pia alitowa Laki mbili kwa Mr & Miss Jam Session kwaajili ya kuwawezesha kufanya shopping za mavazi yao.
Tags:

About author

Curabitur at est vel odio aliquam fermentum in vel tortor. Aliquam eget laoreet metus. Quisque auctor dolor fermentum nisi imperdiet vel placerat purus convallis.

0 comments

Leave a Reply